Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikwazo dhidi yetu vitadhoofisha jitihada zetu kufikia malengo ya SDG's:Mugabe

Vikwazo dhidi yetu vitadhoofisha jitihada zetu kufikia malengo ya SDG's:Mugabe

Kikao cha Baraza Kuu kimeingia siku ya pili, na mmoja wa waliozungumza ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akisema uwezo wa nchi yake kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG's ifikapo mwaka 2030 utakuwa mgumu, endapo vikwazo vya kiuchumi na kifedha dhidi ya nchi yake vitaendelea.

Vikwazo hivyo viliwekwa miaka 16 iliyopita, na amesema waliofanya uamuzi huu wa kuiadhibu nchi yake, wangependelea kuiona nchi hiyo inakidhi matakwa yao, kwa gharama ya wananchi wake waliowengi, na hivyo akasema....

(Sauti ya Mugabe)

"Narejelea wito wangu kwa Uingereza na Marekani na washirika wake, kuondoa vikwazo hivi haramu na visivyo halali dhidi ya nchi yangu na watu wake. Sisi sote ni lazima tushikamane katika ahadi zetu za ajenda ya 2030 ambapo sote tulikubaliana kuachana na vikwazo na badala yake kufanya mazungumzo".

Pia amemshukuru Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa kazi yake nzuri katika kuendeleza uhuru, maendeleo, amani na ulinzi katika bara la Afrika, na zaidi ya hayo, katika uongozi wake katika kuhamasisha wadau wote wakati wa mlipuko wa Ebola Afrika.