Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo endelevu ni muhimu kwa amani ya kudumu:Ban

Maendeleo endelevu ni muhimu kwa amani ya kudumu:Ban

Kila mwaka katika siku ya kimataifa ya amani Umoja wa mataifa unatoa wito kwa pande zote kinzani duniani kuweka silaha chini na kutekeleza saa 24 za usitishaji wa uhasama. Ikiwa ni ishara ya siku bila mapigano ambalo ni kumbusho muhimu sana kwamba vita vinaweza na ni lazima vikome.

Katika ujumbe wake maalumu wa siku hii ya kimataifa ya amani ambayo kila mwaka huwa Septemba 21, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema amani ni zaidi ya kuweka silaha chini ni kujenga jamii ya kimataifa ambayo watu wataishi wakiwa huru bila umasikini na kushirikiana faida za mafanikio.

Hivyo ni kukua kwa pamoja na kusaidiana kama familia ya kimataifa. Kauli mbiu yam waka huu inaainisha malengo 17 ya amaendeleo endelevu yaani SDG, kama ujenzi wa msingi kwa ajili ya amani.

Ban amesema ajenda hiyo ya 2030 ni muongozi wa kuzuia migogoro kuzuka kwa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.

Ameziasa nchi kutekeleza malengo hayo 17 akisisitiza kuwa ni muhimu kwa amani ya kudumu na vyote vitategemea kuheshimu haki za binadamu, na inahitajika katika kuilinda dunia yetu.