Nigeria imepiga hatua dhidi ya Boko Haram: Rais Buhari
Nigeria hivi sasa inakumbwa na vikwazo vingi kama ugaidi wa Boko Haram, rushwa na mabadiliko ya tabianchi. Hayo ni kwa mujibu wa Rais Muhammadu Buhari wakati wa hotuba yake ya pili katika kikao cha baraza kuu tangu kuchaguliwa kuwa rais wa Nigeria.
Amesema wakati huu ambapo ugaidi unaathiri ulimwengu mzima na changamoto za kukabiliana nao ni kubwa, lakini....
(Sauti ya Buhari)
"Nigeria imesonga mbele mno katika kukabiliana na Boko Haram , ambapo uwezo wake wa kufanya mashambulizi ya kigaidi umepunguzwa makali. Katika miezi michache iliyopita , operesheni zao zimesalia kuwa za hapa na pale na zenye kutumia vifaa vya mlipuko vya kutengenezwa na kulenga maeneo dhaifu ".
Halikadhalika amesema mabadiliko ya tabianchi yameathiri nchi hiyo, na madhara yake yanaonekana katika ziwa Chad ambapo maji yanakauka, na kuathiri takriban milioni 30 wakazi wa eneo hilo. Vile vile Nigeria imejizatiti katika kusafisha eneo lenye mafuta la Ogoni kwenye bonde la mto Niger.