Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna habari njema na mbaya kuhusu hukumu ya kifo:Somonivic

Kuna habari njema na mbaya kuhusu hukumu ya kifo:Somonivic

Hivi sasa duniani kote nchi karibu 170 wanachama wa Umoja wa mataifa ama wamefuta hukumu ya kifo au hawaitekelezi. Hayo yamesemwa na Ivan Šimonoviæ msaidizi wa Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kabla ya mjadala wa ngazi ya juu Jumatano kwenye Umoja wa mataifa kuhusu kuachana na hukumu ya kifo amesema kuna habari njema na habari mbaya

(SAUTI YA SIMONOVIC 1)

"Kwa upande wa habari njema , haijawahi kutokea katika historia ya mwanadamu kuwa nan chi nyingi zilizofuta hukumu ya kifo kama sasa, lakini kwa upande mwingine ukilinganisha mwaka 2015 na mwaka 2014, kulikuwa na ongezeko ya idadi ya hukumu za kifo zilizotekelezwa hivyo ni habari mchanganyiiko”

Kisha ameeleza sababu zilizochangia ongezeko hilo

(SAUTI SIMONOVIC 2)

"Nadhani hofu ya ugaidi na jaribio la kukabiliana kwa mafanikio tatizo la mihadarati kwa njia Fulani vimechagiza mwenendo mbaya unaotukabili”