Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoshirikiana kwa wanawake na wanaume ni pigo kwa maendeleo Uganda

Kutoshirikiana kwa wanawake na wanaume ni pigo kwa maendeleo Uganda

Wakati dunia imeadhimisha mwaka mmoja tangu kupitishwa kwa malengo ya maendeleo endelevu SDGs au ajenda 2030, lengo namba tano linaloangazia kumaliza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana kote ulimwenguni linasongeshwa huku likikumbwa na changamoto kwingineko.

Mathalani lengo hilo linatilia mkazo umuhimu wa kuimarisha usawa wa majukumu ndani ya familia kama kitu ambacho kinastahili kitaifa. Hata hivyo nchini Uganda kuna malalamiko kuwa baadhi ya wanaume hukwepa majukumu yao muhimu na hivyo kuleta hali ya vuta nikuvute katika jamii. Basi ungana na John Kibego katika makala hii kupata uelewa zaidi.