Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama wa wakimbizi ni muhimu kwenye vituo vya mapokezi:UNHCR

Usalama wa wakimbizi ni muhimu kwenye vituo vya mapokezi:UNHCR

Hofu kubwa dhidi ya usalama wa waomba hifadhi nchini Ugiriki imeelezwa na Umoja wa Mataifa , baada ya kuzuka moto mkubwa kwenye kituo cha mapokezi kilichofurika umati wa watu.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa hakuna aliyepoteza maisha au kujeruhiwa vibaya katika ajali hiyo ya moto kwenye kituo cha Moria, kisiwani Lesvos, ambapo Shirika la Umoja wa M  ataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linasema ulianza baada ya kuibuka kwa ugomvi miongoni mwa wakazi.

Kwa mujibu wa William Spindler msemaji wa UNHCR, tukio hilo linathibitisha umuhimu wa usalama kwenye vituo vya mapokezi

(SAUTI YA SPINDLER)

“UNHCR imerejea kutoa wito wa usalama na utekelezwaji wa sheria ili kuongeza ulinzi kwa wakimbizi, wahamiaji, wafanyakazi wa misaada na wafanyakazi wa kiraia kwenye vituo hivyo. Maisha duni, ukichanganya na hali ya sintofahamhamu mara kwa mara huchochea hali ya kukata tamaa na kuchanganyikiwa miongoni mwa waomba hifadhi nchini Ugiriki.”

UNHCR inasema kulikuwa na watu 4,400 wanaoishi kituoni hapo wakati moto ulipozzuka, na idadi hiyo ni kubwa kuliko uwezo wa wa kituo hicho.