Skip to main content

Pazia la mkutano wa wakimbizi na wahamiaji lafungwa

Pazia la mkutano wa wakimbizi na wahamiaji lafungwa

Mkutano wa siku moja wa ngazi ya juu kuhusu wakimbizi na wahamiaji umefikia ukingoni jioni ya Jumatatu baada ya mjadala wa siku nzima ulioleta simulizi, shuhuda na mipango ya kusaka suluhu la kudumu la makundi hayo kwa mujibu wa azimio la New York, lililopitishwa asubuhi.

(Wimbo-Imagine)

Kibao hiki Imagine cha John Lennon kilitangulia hotuba ya kufunga mkutano huo.

Kikitumbuizwa na tena kwa ushirikiano kati ya mkewe Yoko Onno na mchezesha muziku mashuhuri David Guetta wa Ufaransa kwa uratibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kibao kinaeleza fikiria dunia ambamo kwayo kila mtu anaishi kwa amani..

Na hatimaye Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson akachukua nafasi yake kufunga mkutano huo akisema baada ya simulizi na shuhuda kutoka kwa wakimbizi juu ya madhila wanayopitia, au mbinu bunifu za kusaidia wakimbizi na wahamiaji sasa kilichobakia..

“Lazima tufanye kazi kwa pamoja zaidi hivi sasa kuliko hapo awali. Hali iliyoko sasa inahitaji udharura na hatua za haraka.”