Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhalifu wa kikatili ni dharura ya kimataifa: Adams

Uhalifu wa kikatili ni dharura ya kimataifa: Adams

Mauaji ya kimbari, uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu au ule uitwao uhalifu wa kikatili imekuwa ni dharura ya kimataifa.

Hayo ni kwa mujibu wa Simon Adams, mkurugenzi mtendaji wa kituo cha kimataifa cha wajibu wa kulinda , ambaye anahutubia leo Jumanne mkutano kuhusu suala hilo kwenye kamao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Wataalamu na viongozi wa dini mbalimbali kutoka kote duniani wanajadili jukumu la dini katika kuzuia uhalifu wa kikatili.

Bwana Adams anaelezea uhusiano uliopo baina ya dini na kuzuia uhalifu

(SAUTI YA ADAMS)

“Mfano katika sehemu tiofauti duniani ambapo dini imetumika kugawanya watu mfano ni jumukumu la kundi linaloitwa Islamic State na kundi kama Boko Haram, nadhani viongozi wa dini wanaweza kuwa muhimu sana hususani katika jamii zilizogawanyika kama Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako dini imekuwa na jukumu muhimu la kusaidia kuwaleta watu pamoja badala ya kuchagiza siasa za mapanga”.