Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda sasa ni taifa la 8 kuhifadhi wakimbizi wengi duniani

Uganda sasa ni taifa la 8 kuhifadhi wakimbizi wengi duniani

Leo hii Uganda imeelezwa kuwa ni taifa la 8 duniani kwa kuhifadhi idadi kubwa ya wakimbizi ambapo kufikia mwisho wa mwaka itakuwa na wakimbizi zaidi ya 810,000.

Licha ya changamoto inazokabiliana nazo kwa kupokea wakimbizi wengi , waziri wa misaada kwa ajili ya maandalizi ya majanga na wakimbizi Hilary Onek , akizungumza kwenye mjadala kuhusu wakimbizi na wahamiaji amesema,  itaendelea kuhakikisha haki za wakimbizi zinaheshimiwa pamoja na kuendelea kuwaorodhesha wakimbizi wote kutoka Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Burundi.

Ameongeza kuwa pia watatoa vitambulisho kwa wakimbizi wote, kusajili watoto wakimbizi waliozaliwa nchi humo na kuhakikisha kuwa wakimbizi hao wanapata huduma za afya na elimu. Bwana Oken amesema serikali yake imechukuwa mtazamo madhubuti zaidi wa kuwapatia wakimbizi ardhi kwa ajili ya makazi na kilimo, yenye thamani ya doma milioni 50.

Na kwa sasa Uganda imeomba mkono kwenye bank ya dunia ambao utasaidia kushughulikia pengo la maendeleo katika makazi ya wakimbizi.