Skip to main content

Misaada ya kibinadamu haifai kuwa mambo ya kisiasa-Pinheiro

Misaada ya kibinadamu haifai kuwa mambo ya kisiasa-Pinheiro

Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marekani na Urusi lazima yafuatwe kwa haraka.

Hiyo ni kauli ya mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Mataifa inayochunguza Syria, Paulo Pinheiro akiwasilisha ripoti yake ya 15  mbele ya Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Amewaeleza wanachama wa baraza la haki kibinadamu kuwa misaada ya kibinadamu haifai kuwa mambo ya kisiasa.

Amesema kila siku vita inazidi nchini Syria, na kuwa ni siku nyingine ya mateso kwa wananchi wa taifa hilo.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa wiki moja ya kusitishwa kwa uhasama ilileta matumaini kwani ilipunguza idadi ya majeruhi.

Hata hivyo Bwana Pinheiro amewakumbusha jinsi ahadi ya usitishaji wa uhasama ilvyotupiliwa mbali na mgogoro kulipuka tena.

(Sauti ya Pinheiro)

"kauli nyingine ya kusitisha uhasama iliyofikiwa mwezi wa Febrauari ilisaidia kidogo kwa sababu Syria uwanja wa vita wa nchi kadhaa zinazohusika na kwamba ni wananchi wanaoteswa na ukiukaji wa sheria za kibinadamu na  mbinu za kuzingirwa kuwa hazifai na sheria dhidi yao ni sawa ni zile sheria dhidi ya vifaa vya vita''.

Hoja ya kufikishwa kwa msaada wa kidharura kwa watu 600,000 bado ni jambo ambalo linazidi kuwa changamoto katika usisitishaji wa uhasama.

Vilevile mchunguzi huyo amesema  mbinu ya kuorodhesha madhila bado inaaendelea sanjari na taarifa kutoka serikali ya Syria kuwa ISIL imechimba kaburi ya halaiki huko Palmyra.