Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutambua mchango wa wakimbizi na wahamiaji ni muhimu sana-Somalia

Kutambua mchango wa wakimbizi na wahamiaji ni muhimu sana-Somalia

Somalia inasema wakimbizi na wahamiaji wana mchango mkubwa katika jamii watokazo na waendako, tofauti na fikra za wengi kwamba watu hao ni chanzo cha madhila hasa kwa jamii zinazowapokea.

Hayo ni kwa mujibu wa mshauri wa kitaifa wa Somalia kuhusu masuala ya wakimbizi na wakimbizi wa ndani, Bwana Ahmed said Farah, aliyeiwakilisha nchi yake katika mjadala wa ngazi ya juu kuhusu wakimbizi na wahamiaji Jumatatu.

Katika mahojiano maalumu na Flora Nducha wa idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa Bwana Farah anaanza kwa kueleza umuhimu wa mkutano huu wa wakimbizi na wahamiaji

(MAHOJIANO NA AHMED SAID FARAH)