Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuo Kikuu cha Oxford chataja sababu za wakimbizi kujitegemea Uganda

Chuo Kikuu cha Oxford chataja sababu za wakimbizi kujitegemea Uganda

Utafiti uliofanywa nchini Uganda na Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza umebaini kuwa mbinu ya kuwawezesha wakimbizi kujitegemea inasadia pia wenyeji.

Akiwasilisha utafiti wake wakati wa kikao kuhusu kuwezesha wakimbizi kujitegemea, kando mwa kikao cha ngazi ya juu kuhusu wakimbizi na wahamiaji mjini New York, Marekani, Profesa Alexander Bett ametoa mfano..

(Sauti ya Profesa Bett)

“Mjini Kampala, asilimia 21 ya wakimbizi wanaendesha biashara inayoajiri angalau mtu mwingine na ukiangalia walioajiriwa, asilimia 40 ni raia wa Uganda. Kwa maneno mengine, wakipatiwa fursa, wakimbizi wanatengeneza ajira kwa raia.”

Profesa Bett amesema pamoja na fursa ya biashara wamebaini mambo mengine yanayochochea wakimbizi kujitegemea ni kupata miundombinu kama ile ya mawasiliano ya intaneti, barabarani halikadhalika, elimu akisema..

(Sauti ya Profesa Bett)

“Kwa mkimbizi, kila mwaka wa nyongeza wa elimu ya msingi huongeza kipato cha mwaka kwa angalau asilimia Mbili nukta Nne, na mapato hayo yanaongezeka kadri hatua inavyopanda. Hivyo ni lazima tuhakikishe elimu ya sekondari na zaidi ya hapo kwa wakimbizi.”