Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Eliasson aipongeza IOM kuwa sehemu ya familia ya UM

Eliasson aipongeza IOM kuwa sehemu ya familia ya UM

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amelikaribisha na kulipongeza shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kuingia rasmi katika familia ya Umoja wa mataifa.

Amesema shirika hilo kwa miaka 65 limekuwa likifanya kazi kubwa na linastahili kuingia kwenye familia ya Umoja wa mataifa . Muafaka mpya baina ya mashirika hayo mawili amesema utanufaisha pande zote, na la msingi zaidi utawafaidi wahamiaji nan chi wanachama.

Ameongeza kuwa changamoto ni kubwa , masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa yanavuka mipaka, lakini kuna umuhimu wa kuhakikisha usalama, utaratibu na uhamiaji unaowajibika, hasa kwa kuzingatia haki za binadamu na wajibu wa kibinadamu.