Kenya yataka usaidizi wa kimataifa kwa wakimbizi
Nayo Kenya moja ya nchi inazohifadhi wimbi kubwa kabisa la wakimbizi imewakilishwa na Makamu wa Rais William Ruto kwenye mjadala huo.
Akihojiwa na idhaa hii, Bwana Rutto amesema kuna changamoto kama vile kugomebea rasilimali kati ya wakimbizi na wenyeji, na pia usalama lakini,
(Sauti ya Ruto)

Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu Ban. Picha;UN Photo/Rick Bajornas
Bwana Ban amepongeza ukarimu wa Kenya wa kuendelea kusaka suluhu ya kudumu ya amani katika nchi hizo.
Halikadhalika ameshukuru Kenya kwa dhima yake adhimu ya kusaidia wakimbizi na amekaribisha azma ya nchi hiyo ya kuendelea na wajibu wake huo wa kimataifa hususan hoja ya kurejeshwa kwa wakimbizi.
Katibu Mkuu ametumia pia fursa hiyo kuisihi Kenya kuridhia mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi.