Skip to main content

Azimio kuhusu wakimbizi na wahamiaji lapitishwa New York:

Azimio kuhusu wakimbizi na wahamiaji lapitishwa New York:

Leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika mkutano wa ngazi ya juu ambao tayari umepitisha azimio la New York kuhusu wakimbizi na wahamiaji. Azimio hili linawajibisha kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa kuwatendea haki wakimbizi na wahamiaji. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Katika hotuba yake kabla ya kupitishwa kwa azimio, wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema, tusiangalie suala la wakimbizi na wahamiaji kama mzigo bali rasilimali kwani..

(Sauti ya Ban)

" Wanaleta uwezo mkubwa, tukiwapa fursa ya kuifungua. Ni lazima tubadili majadiliano yetu kuhusu wakimbizi na wahamiaji .Ni lazima kuongea nao. Maneno yetu na mazungumzo nao yana umuhimu."

Naye Rais wa Baraza Kuu, Peter Thomson amesema wakati huu ulimwengu unashuhudia wimbi kubwa la wakimbizi ambalo halikuonekana tangu vita vikuu ya pili ya dunia, akisema...

(Sauti ya Thomson)

"Zaidi ya nusu ya wakimbizi duniani ni watoto , ambao wengi wao hawawezi kupata elimu.Wanawake na wasichana ndio wanaokumbwa zaidi na mazingira magumu , na mara nyingi wakikumbwa na madhara ya kimwili, aina nyingi ya ubaguzi, na ukosefu wa upatikanaji wa huduma za msingi. Nimeogopeshwa zaidi kwamba watu wengi wanaokimbia kutafuta usalama , wanakutana na hulka za uadui na chuki . Natumai kampeni mpya ya Katibu Mkuu ya kukabiliana na ubaguzi wa wageni itasaidia kuondokana na hulka hii".

Kisha mwenyekiti mwenza wa kikao, Peter Thomson akawasilisha rasimu ya azimio

(Nats...nyundo....)

Sauti ya kugongwa kwa nyundo ikiashiria kwamba rasimu ya azimio hilo sasa imepitishwa......

(Nats Makofi...)

image
Naye Kamisha mkuu wa wakimbizi Fillipo Grandi akizungumza baada ya kutipitishwa kwa rasimu ya azimio hilo na nchi 193 amesema azimio hilo ambalo litazibana nchi wanachama chini ya sheria za kimataifa pia...

(SAUTI YA FILLIPO GRANDI)

“Linadhihirisha dhamira ya pamoja ya jumuiya yote ya kimataifa , kushirikiana kwa pamoja katika njia mpya na za pamoja kukabiliana na hali ya wakimbizi na wahamiaji, kuwa inayoweza kutabirika zaidi, inayoweza kusaidika na yenye rasilimali zaidi”