Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaingiza msaada kwa ndege Uganda, huku maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini wakiwasili

UNHCR yaingiza msaada kwa ndege Uganda, huku maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini wakiwasili

Maelfu ya watu wanaokimbia vita na ukiukwaji wa haki za binadamu Sudan kusini wameanza kufaidika na operesheni kubwa ya msaada wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Grace Kaneiya na taarifa zaidi

(TAARIFA YA GRACE)

Hii ni kufuatia kuwasili kwa ndege aina ya Boeing 747 mjini Entebe Uganda siku ya jumapili ikiwa imebeba tani zaidi ya 100 na msaada wa dharura.

Msaada huo ni pamoja na maelfu ya vyandarua vya mbu, magodoro, mahema, vifaa vya kupikia, na taa zinazotumia mwanga wa jua ambavyo vitafikishwa kwenye makazi ya wakimbizi ya Adjumani, Arua na wilaya ya Kiryandongo , pamoja na kwa wale walioko kwenye makazi mapya ya Bidibidi mjini Yumbe.

Ndege hiyo imekabidhiwa kwa UNHCR na makamu wa Rais wa Emarati kwa niaba serikali ya Emarati baada ya kusikia madhila yanayowakabili wakimbizi wa Sudan Kusini.