Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kuingizwa ndani ya UM ni heshima kubwa kwa wahamiaji- Swing

IOM kuingizwa ndani ya UM ni heshima kubwa kwa wahamiaji- Swing

Hatimaye shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM baada ya kuhudumia wahamiaji kwa miaka 65, leo limejumuishwa rasmi katika familia ya Umoja wa Mataifa na kuwa shirika la Umoja wa Mataifa la wahamiaji.

Shughuli za kutia saini hatua hiyo kwa mujibu wa azimio namba A70/290 imefanyika baada ya kupitishwa kwa azimio la New York kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza baada ya tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa IOM William Swing amesema

(Sauti ya Swing)

 “Kwa hiyo kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 71, Umoja wa Mataifa sasa una shirika lake la kuhudumia wahamiaji. Hii ni heshima ya kipekee kwa shirika letu, na naamini ni mafanikio ya dhati kwa wahamiaji, nchi wanachama, na zaidi ya yote kwa mkutano huu.”