Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio kuhusu wakimbizi na wahamiaji lapitishwa na baraza kuu UM

Azimio kuhusu wakimbizi na wahamiaji lapitishwa na baraza kuu UM

Kikao cha ngazi ya juu cha 71 cha baraza kuu kimeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York.

Nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa wanaojadili mustakhbali wa mamilioni ya wakimbizi na wahamiaji wamepitisha azimiokwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji linalozingatia masuluama makuu manne, kwanza kuhakikisha usalama, utu , haki za binadamu na uhuru kwa watu hao bila kujali hali yao ya ukimbizi au uhamiaji.

Akizungumzia kuhusu azimio hilo ambalo litazibana nchi wanachama chini ya sheria za kimataifa Kamisha mkuu wa wakimbizi Fillipo Grandi amesema azimio hilo pia

(SAUTI YA FILLIPO GRANDI)

“Linadhihirisha dhamira ya pamoja ya jumuiya yote ya kimataifa , kushirikiana kwa pamoja katika njia mpya na za pamoja kukabiliana na hali ya wakimbizi na wahamiaji, kuwa inayoweza kutabirika zaidi, inayoweza kusaidika na yenye rasilimali zaidi”

Azimio hilo la kisiasa  linatambua  pia mchango mkubwa unaofanywa na wakimbizi na wahamiaji katika masuala ya maendeleo. Na linatoa muda hadi mwaka 2018 kutakapofanyika mkutano wa kimataifa wa wahamiaji ambao unatarajiwa kpitisha mkakati wa kimataifa kuhusu suala hilo.