Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tetemeko la ardhi nchini Tanzania

Tetemeko la ardhi nchini Tanzania

Tarehe 10 mwezi huu wa Septemba majira ya alasiri, tetemekeo la ardhi lenye ukubwa wa 5.9 katika kipimo cha richa lilipiga ukanda wa ziwa Victoria na kuleta madhara zaidi mkoani Kagera nchini Tanzania.

Tetemeko hilo lilisababisha watu 17 kufariki dunia, 253 walijeruhiwa huku 53 walilazwa hospitali kwa matibabu. Halikadhalika mali ziliharibika ambapo Umoja wa Mataifa umesema miongoni ni majengo 840 na nyumba 5,000 ambazo zilibomoka. Je hali ikoje hivi sasa.

Nicholous Ngaiza wa radio washirika Kasibante FM mkoani Kagera nchini Tanzania ametembelea waathirika kufahamu mahitaji yao sambamba na mtazamo wa Umoja wa Mataifa kuhusu umuhimu wa hatua za kudhibiti majanga.