Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wekeni mitutu chini kwa ajili ya kudumisha amani:Ban

Wekeni mitutu chini kwa ajili ya kudumisha amani:Ban

Leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunaadhimishwa siku ya amani duniania ambayo kila mwaka huwa Septemba 21,. Hafla maalumu imeongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akisema kuendeleza ujenzi wa amani ndio sababu ya uwepo wa Umoja wa Mataifa. Taarifa zaidi na Flora Nducha.......

(Taarifa ya Flora...)

Nats..

Tumbuizo katika bustani za Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani likiashiria maadhimisho ya siku ya amani, buruidani hiyo ikaambatana na hotuba mbalimbali, Katibu Mkuu Ban alianza kwa kuwashukuru wajumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa ambao wamehudhuria hafla hiyo na kisha akatoa wito ....

(Sauti ya Ban)

"Katika maadhimisho ya siku hii ya amani duniani, natoa wito kwa wapiganaji duniani kote, kuweka chini silaha zao, na kushuhudia siku ya kusitisha mapigano duniani na kupinga machafuko"

Na Kisha akagonga kengele ya amani…..

(Kengele)

image
Katibu Mkuu Ban Ki-moon akigonga kengele ya amani. Picha:UN Photo/Rick Bajornas
Naye Rais wa Baraza Kuu la 71 Peter Thomson akasema kauli mbiu ya mwaka huu...

(Sauti ya Thomson)

"Malengo ya maendeleo endelevu, matofali yanayojenga amani yana umuhimu zaidi katika siku hii. Malengo yaliyokubaliwa na ulimwengu mzima kwa watu, sayari na ustawi, inaweka bayana mpango kamilifu utakaotusaidia kuondokana na mizizi ya migogoro"