Skip to main content

Watu milioni moja wakimbia Sudan Kusini, UNHCR

Watu milioni moja wakimbia Sudan Kusini, UNHCR

Idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini waliokimbilia nchi jirani sasa imefikia milioni moja, wakiwemo 185,000 waliokimbia mzozo mpya ulioibuka jijini Juba mnamo July nane mwaka huu, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. John Kibego na maelezo zaidi.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Kwa mujibu wa UNHCR, idadi hiyo inatia Sudan Kusin katika orodha ya nchi zenye mizozo iliyosababisha wtu zaidi ya milioni moja kukimbia nchi zao ambazo ni Syria, Afghanistan na Somalia.

Mapigano kati ya wnajeshi wanaomtii Makamu Raisi wa zamani Riek Machar na jeshi la serikali ya Sudan Kusini yamelazimisha maelfu kukimbia makwao hivi karibuni, huku zaidi wa milioni 1.61 wakisalia kama wkaimbizi wa ndani.

Uganda ndio imepokea idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Sudan Kisini ikiwa na takriban laki nne ikifuatua na Ethiopia yenye wakimbizi 292,000 na Sudan inayohifadhi 247,317.

Wakati huohuo, UNHCR, imetoa ombi la 80% ya dola miloni 701 za kutekeleza operesheni zake za za kushughulikia wakimbizi wa Sudan Kusini