Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya Kibinadamu yazidi kuwa mbaya Mashariki mwa Ukraine:Ripoti ya UM

Hali ya Kibinadamu yazidi kuwa mbaya Mashariki mwa Ukraine:Ripoti ya UM

Kumekuwa na ongezeko kubwa la majeruhi katika migogoro ya wenyewe kwa wenyewe mashariki mwa Ukraine katika kipindi cha kiangazi. Ripoti mpya kutoka kwa wataalamu wa maswala ya haki za binadamu chini Ukraine kati ya mwezi mei na Agosti mwaka huu inasema  kumetokea visa188 vya majeruhi, ikiwemo vifo vya watu 28 ambayo ongezeko la asilimia 66 likiwa ni ongezeko kubwa ukilinganisha na miezi mitatu iliyopita.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya waasi na serikali vimedumu tangu Aprili mwaka 2014 na vimeshasababisha vifo vya watu 9,640 mapak sasa.

Kamishina mkuu wa  haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa  Bw. Zeid Ra’ad Hussein amesema japo hali ipo shwari kutokana na makubaliano ya kusitisha vita ya tarehe Mosi september,kuna wasiwasi hali yaweza kuchafuka tena muda wowote.