Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumieni #UN4RefugeesMigrants kuibua mabadiliko: Karen AbuZayd

Tumieni #UN4RefugeesMigrants kuibua mabadiliko: Karen AbuZayd

Wakati wa kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo wiki ijayo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR litatumia fursa hiyo kuangazia suala la wakimbizi na wahamiaji.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani, Karen AbuZayd, ambaye ni mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkutano huo unaosaka mbinu za kushughulikia wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji amesema watapitisha azimio.

Amesema azimio hilo linaangazia haki za wakimbizi na wahamiaji katika nyanja zote, na mataifa 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa yanatarajiwa kuridhia na akaongeza kuwa hiyo itakuwa ni hatua moja.. ...

(Sauti ya Karen)

"Lakini matokeo halisi yataonekana katika utekelezaji, kwa mfano watu wanapohamia sehemu yenye usalama zaidi, nchi inayowahifadhi kupokea msaada mkubwa, na wasichana na wavulana wakimbizi zaidi wanahudhuria shule"

Bi. Karen ametoa wito kwa kila mmoja kupigia debe siku hii kabla ya mkutano Jumatatu, kama njia ya kuwahimiza viongozi wao kulinda haki za wakimbizi kwa kutumia #UN4RefugeesMigrants kwenye mitandao yao ya kijamii. Kufahamu zaidi tembelea tovuti http://refugeesmigrants.un.org/.