Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda ni mfano kwa usaidizi kwa wakimbizi #UN4RefugeesMigrants

Uganda ni mfano kwa usaidizi kwa wakimbizi #UN4RefugeesMigrants

Mkutano kuhusu wakimbizi na wahamiaji utafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 19 mwezi huu. Lengo ni kuangazia ni mikakati gani ichukuliwe ili madhila ya wakimbizi yaweze kushughulikiwa kule waliko na hatimaye amani irejee makwao na hivyo waweze kurejea nyumbani.

Uganda imepokea wakimbizi zaidi ya 300,000 kutoka Sudan kusini, Burundi na DR Congo. Miongoni mwao,  200,000 wametoka Sudan Kusini. Licha mzigo huo wa wakimbizi, Uganda imetajwa kuwa ni nchi ambayo kwayo  hatua zake za usaidizi kwa wakimbizi zimekuwa ni mfano wa kuigwa. Je nini wamefanya?

Rosemary Musumba wa Idhaa hii amezungumza na Mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Uganda Bornwell Kantande. Hapa Bwana Kantende anaanza kwa kuelezea kile ambacho serikali ya Uganda inafanya kusaidia wakimbizi.