Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

India yaipiku Marekani soko la intaneti- Ripoti

India yaipiku Marekani soko la intaneti- Ripoti

India imeipiku Marekani na kuwa nchi ya pili duniani kwa idadi kubwa ya soko la mtandao wa intaneti hususan majumbani.

Taarifa hizo zimo kwenye ripoti mpya ya hali ya upatikanaji wa mtandao ulimwenguni iliyotolewa hii leo ikieleza kuwa India imechukua nafasi hiyo ikiwa na watu Milioni 333 ambapo namba moja ni China.

Idadi ya watu wenye mtandao wa intaneti majumbani nchini China ni milioni 720.

Hata hivyo nchi mbili hizo zenye idadi kubwa ya watu, zinachangia asilimia 55 ya watu wote ulimwenguni ambao hawajaunganishwa na mtandao huo wa mawasiliano.

Ripoti hiyo inasema wakati nchi tajiri zimeunganishwa zaidi kimtandao, bado nchi maskini zina changamoto hasa katika sekta ya elimu na afya.

Watu bilioni 3.9 ulimwenguni hawajaunganishwa na mtandao wa intaneti.