Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia kupitisha sera ya ubinadamu zaidi kwa wakimbizi na wahamiaji

Viongozi wa dunia kupitisha sera ya ubinadamu zaidi kwa wakimbizi na wahamiaji

Viongozi wa dunia wanajiandaa kupitisha sera yenye mtazamo wa kibinadamu zaidi katika kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji duniani amesema afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa.

Balozi David Donaghue wa Ireland ni mwenyekiti mwenza wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya wakimbizi na wahamiaji uliopangwa kufanyika Jumatatu ya Septemba 19.

Wakuu wa nchi na serikali wanatarajiwa kupitisha sera mpya za kimataifa na mikakati kuhusu wakimbizi na wahamiaji.

Kuna wahamiaji zaidi ya milioni 244 na wakimbizi zaidi ya milioni 21 kote duniani. Balozi Donaghue anafafanua anamaanisha nini kuhusu sera za ubinadamu zaidi..

(SAUTI YA DONAGHUE)

“Ubinadamu maanayake ni kujaribu kuhakikisha kwamba watu ambao wamefurushwa kutoka mwakao wanapokelewa kwa njia ya kiutu na heshima wanaostahili, katika nchi wanakopitia na mahali wanakowenda kupewa kwa mfano fursa za afya, elimu, fursa za kazi ili waangaliwe kwa mahitaji yao ya haraka ya kibinadamu lakini pia waendelee kupata msaada wa maendeleo.”

Ameongeza kuwa hiyo ndio mada itakayotamalaki kwenye mkutano wa wiki ijayo sanjari na kuangalia kwa kina mahitaji ya haraka na msuluhu ya muda mrefu kwa mamilioni ya wakimbizi na wahamiaji.