Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi wa Rais na wabunge DRC kufanyika siku moja

Uchaguzi wa Rais na wabunge DRC kufanyika siku moja

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, makubaliano yamefikiwa katika mjadala wa kitaifa kuwa uchaguzi wa Rais, wabunge na wawakilishi wa majimbo ufanyike siku moja.

Msimamizi wa mashauriano hayo kutoka Muungano wa Afrika, AU, Edem Kodjo ametangaza hayo ikiwa ni siku chache baada ya upande wa upinzani kueleza jumatatu kuwa unajitoa kwa kuwa uchaguzi wa Rais ulipendekezwa kufanyika baadaye.

(Sauti ya Edem)

“Uchaguzi wa rais, wabunge na wawakilishi wa majimbo utafanyika siku moja. Chaguzi hizi zitaunganishwa na zile za mitaa iwapo uwezo wa kiufundi na kifedha utaruhusu."

Hata hivyo tarehe ya uchaguzi huo mkuu ambao kwa mujibu wa Bwana Kodjo serikali ya DRC imesema itafadhili yenyewe, bado haijapangwa.