Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CERF yatenga dola milioni 10 kusaidia watu zaidi ya 200,000 Chad

CERF yatenga dola milioni 10 kusaidia watu zaidi ya 200,000 Chad

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa Stephen O’Brien, ameidhinisha dola milioni 10 kutoka mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF kwa ajili ya kusaidia masuala ya kibinadamu Chad. Grace Kaneiya na taarifa zaidi

(TAARIFA YA GRACE)

Fedha hizo zitatumika kutoa msaada muhimu unaohitajika katika majimbo manne ya Kusini mwa nchi hiyo kili kukidhi mahitaji ya wakimbizi 210,000 na watu wanaorejea nyumbani kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na jamii zilizokuwa zinawahifadhi.

Kwa mujibu wa jumuiya ya kimataifa hali katika majimbo ya Moyen-Chari, Mandoul, Logone Oriental na Logone Occidental, Kusini mwa Chad kwenye mpaka na CAR, ni ya kutia hofu ikiambatana na kuzorota kwa uhakika wa chakula, huku wadau wa misaada wa kimataifa wakianza kuondoka taratibu kutokana na ukosefu wa fedha.

Kwa ujumla miradi saba inayofadhiliwa na CERF itatoa msaada wa kuokoa maisha unaohitajika nchini humo