Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya imejizatiti kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDG’s:UNDP

Kenya imejizatiti kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDG’s:UNDP

Serikali ya Kenya imepongezwa kwa jitihada zake za kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu hayasalii kuwa ndoto tu, bali yanashuhudiwa kwa vitendo.

Hayo yamesemwa na Siddharth Chatterjee, mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya ambaye pia ni mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP.

Akizungumza katika hafla maalumu ya uzinduzi wa kitaifa wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s mjini Nairobi Kenya bwana Chatterjee amesema

(SAUTI YA CHARTTERJEE)

Kenya imesismama kidete sio tu kuhakikisha mafanikio ya SDG’s, bali pia kuhakikisha malengo hayo yanakumbatiwa na jumuiya ya kimataifa. Na ukiyaangalia kwa undani malengo ya maendeleo endelevu, ni dhahiri kwamba Kenya iko mbela katika kuhakikisha malengo ya SDG’s yanakuwa”

Amesema malengo ya SDG’s yanagusa masuala mbalimbali ikiwemo, maji, makazi, migogoro na usalama mambo ambayo yapo pia katika ajenda ya Afrika ya mwaka 2063. Na kuhakikisha yote hayo yanashughulikiwa na serikali inapaswa kubeba jukumu kubwa.