Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMIL kuendelea kuwepo Liberia hadi mwisho wa mwaka huu

UNMIL kuendelea kuwepo Liberia hadi mwisho wa mwaka huu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa ujumbe wake huko Liberia, UNMIL, hadi tarehe 31 mwezi Disemba mwaka huu.

Uamuzi huo umo kwenye azimio lililopitishwa hii leo kwa kauli moja na wajumbe 15 wa baraza hilo.

Azimio hilo linasema kuongezwa muda wa UNMIL kunatokana na ukweli kwamba hali ilivyo nchini humo bado ni tishio kwa amani na usalama kwenye ukanda husika.

Pamoja na kuongezwa kwa muda, idadi ya kikosi itasalia ile ile ya askari 1,240 na polisi 606.

Baraza hilo limesema mustakhbali wa uwepo wa UNMIL nchini humo utategemea tathmini na mapendekezo ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatakiwa awe amewasilisha ifikapo tarehe 15 Novemba mwaka huu na baraza hilo kuamua mwezi mmoja baadaye.

Muda wa awali wa UNMIL ulikuwa umalizike tarehe 30 mwezi huu.