Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafiri wa meli ni muhimu kwa dunia: IMO

Usafiri wa meli ni muhimu kwa dunia: IMO

Katika kuadhimisha siku ya masuala ya bahari duniani, Katibu mkuu wa shirika la kimataifa la masuala ya bahari IMO, Bwana Kitack Lim amesema, usafiri wa meli ni muhimu sana kwa dunia.

Katika ujumbe wake maalumu kwa siku hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 29, amesema dunia inakabiliwa na changamoto nyingi, kuanzia ugaidi hadi mabadiliko ya tabianchi, hivyo serikali na asasi za kiraia zinasaka mbinu za kuhakikisha maendeleo ya kijamii yanaweza kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya watu inayoongezeka na yanakuwa endelevu.

Ameongeza kuwa IMO na sekta ya usafiri wa meli vinajukumu kubwa katika utekelezaji wa azma hii

(SAUTI YA KITACK LIM)

"Usafiri wa meli ni muhimu kwa dunia, na utasalia kuwa kitovu cha ukuaji wa uchumi duniani hasa wakati huu tukiwa katika mpito kuelekea zama zisizoepukika za maendeleo safi na endelevu."