Skip to main content

Ukwepaji wa sheria utaendelea Sudan Kusini kama hakuna uwajibikaji:UM

Ukwepaji wa sheria utaendelea Sudan Kusini kama hakuna uwajibikaji:UM

Baada ya siku 19 za ziara ya tathimini ya timu ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, hofu iliyopo ni kwamba watu wataendelea kutowajibika endapo hatua madhubuti hazitochukuliwa .

Akizungumza baada ya ziara hiyo mwenyekiti wa wa tume ya haki za binadamu Sudan Kusini Bi Yasmini Sooka ameonya kwamba kilichopo hivi sasa ni ukwepaji wa sheria kuendelea nchini humo endapo hakutakuwa na uwajibikaji.

(SAUTI YA YASMIN)

Ujumbe unaotujia hivi sasa ni kwamba ukwepaji sheria utaendelea Sudan Kusini hadi pale kutakapokuwepo na uwajibikaji. Tunaamini kwamba ziara tunazozifanya nchini tutaweza kufikisha ujumbe kwenye baraza la haki za binadamu na kutoa mapendekezo ya nini kinahitaji kufanyika.”

Timu ya watu watatu ilianzishwa na baraza la haki la binadamu ili kufuatilia na kutoa taarifa ya hali ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini , lakini pia kutoa mapendekezo ya kuboresha hali hiyo.

Timu imefanikiwa kuzuru maeneo ya ulinzi wa raia ya Malakal na Bentiu na kukutana na wanasiasa, viongozi wa kijamii, wakimbizi, wakimbizi wa ndani na wafanyakazi wa misaada kwenye maeneo hayo.