Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zenye maendeleo duni, LDCs, zinapiga hatua:Acharya

Nchi zenye maendeleo duni, LDCs, zinapiga hatua:Acharya

Nchi 48 zenye maendeleo duni kabisa au LDCs, zimeshuhudia maendeleo mazuri , ingawa bado kuna changamoto, zikiwemo hatari mpya na sintofahamu inayotishia hatua za maendeleo zilizopigwa.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyozindiliwa leo kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York kuhusu hali ya mataifa yenye maendeleo duni mwaka 2016. Ripoti hiyo imetolewa na ofisi ya mwakilishi wa mataifa yenye maendeleo duni, nchi zinzoendelea zisizo na bahari na mataifa ya visiwa vidogo yanayoendelea Bwana Gyan Chandra Acharya.

Ripoti hiyo inatanabaisha jinsi mataifa 10 yenye maendeleo duni yalivyopiga hatua , licha ya changamoto znazokabili mataifa hayo kama kuyumba kwa soko la bidhaa, majanga makubwa ya asili, ikiwa ni pamoja na tetemeko la ardhi kwa nchi kama Nepal, vimbunga huko visiwa vya Solomon, Vanuatu na Tuvalu, athari za mbadiliko ya tabia nchi, na milipuko ya magonjwa kama Ebola huko Afrika ya Magharibi ulioambatana na athari nyingi za kiuchumi.

Kwa mujibu wa Acharya, miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni katika matumizi ya simu za mkononi, ambayo yameongezeka karibu mara mbili na fursa ya maji safi ambayo imeongezeka kutoka asilimia 60 2005 hadi asilimia 68 2014. Pia hatua zimepigwa katika kupunguza vifo vya watoto na pengo la uswwa wa kijinsia katika suala la elimu ya msingi.