Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 55 baada ya kuaga dunia UM wayaenzi mema ya Dag Hammarskjöld

Miaka 55 baada ya kuaga dunia UM wayaenzi mema ya Dag Hammarskjöld

Natts…..

Ni muziki maridadi kutoka kwaya ya Umoja wa Mataifa ukitumbuiza katika hafla maalumu ya kumuenzi Dag Hammarskjöld miaka 55 baada ya kifo chake.

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema kwa pamoja dunia inathamini mchango na kusherehekea mafanikio ya Dag Hammarskjöld.

Lakini pia amerejelea wito kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuchagua mtu au watu ili kutathimini taarifa mpya ambazo huenda zikawepo kuhusu mazingira yaliyopelekea kifo cha shupavu huyo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na watu wengine 15.

(SAUTI YA BAN)

"Miongo yote hii baada ya kifo cha Dag Hammarskjold, bado tunahamasishwa na matendo yake na maneno yake ya hekima.”

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika hafla ya kumuenzi Dag Hammarskjöld.(Picha:UM/Rick Bajornas)
Akiangalia watu waliokusanyika kumuenzi shujaa huyo kwenye Umoja wa Mataifa Ban akakumbuka na kunukuu moja ya kauli za Hammarskjold

(SAUTI BAN)

“Haturuhusiwi kuchagua taswira ya hatma yetu, lakini kile tunachokiweka katika hatma hiyo ndio chetu”

Kisha akawaasa kila mmoja kushikamana na kuweka taswira ya pamoja maisha ya utu na dunia bora kwa wote. Akiwataka kuhamasishwa na maisha na kaziza Dag Hammarskjold na kuendeleza malengo na maadili yanayozingatia mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Natts…..