Skip to main content

Eid mbarak waumini wa dini ya kiislamu- Ban

Eid mbarak waumini wa dini ya kiislamu- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewatakia waumini wote wa dini ya kiislamu ulimwenguni Eid Mubarak wakati huu ambapo waumiai hao wanasherehekea sikukuu ya Eid al Haji.

Katika salamu zake Ban amesema sikukuu hii ni siku ya kujitoa kwa ajili ya jambo jema la familia au jamii na kuonyesha upendo na mshikamano kwa wale wahitaji zaidi.

Amesema zama za sasa ambapo jamii zinakumbana na matatizo mengi ikiwemo mapigano, ghaia, mgawanyiko na kukimbia makazi, jamii ishikamane kwa ajili ya utu na kujenga jamii iliyo bora kwa wote.

Katibu Mkuu amewatakia waumini wote wa dini ya kiislamu ulimwenguni heri na baraka katika sikukuu hiyo akisihi pia iwe ya amani.