UM wakaribirisha hatua ya Urusi na Marekani kurejesha usitishaji uhasama Syria:

10 Septemba 2016

Umoja wa Mataifa unakaribisha uelewa ulitangazwa leo na Sergey Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Shirikisho la Urusi na John Kerry, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, kuhusu kurejesha ukomeshaji wa uhasama nchini Syria ili pande husika ziweze kurudi kwenye mazungumzo na upatikanaji wa fursa za kufikisha misaada ya kibinadamu na kuzingatia sheria za wazi kwa ajili ya usimamiaji usitishaji uhasama.

Kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja Mataifa kwa ajili ya Syria Staffan de Mistura, Umoja wa Mataifa unakaribisha pia hatua ya shirikisho la Urusi na Marekani kuwa tayari kufanya kazi pamoja ili kulishinda kundi la Daesh na Al Nusra front.

Umoja wa unatumai kwamba utashi wa kisiasa uliopelekea maelewano hayo utaendelea. De Mistura ameongeaza kuwa unatoa fursa muhimu ambayp wadau wote katika kanda na kwingineko wanapaswa kuitumia ili kuupeleka mzozo wa Syria katika mwelekeo mwingine na kupunguza madhila na mateso yanayowakabili watu wa Syria.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter