Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wakijiandaa na Hija joto la kupindukia na matatizo ya kupumua ndio kipaumbele:WHO

Watu wakijiandaa na Hija joto la kupindukia na matatizo ya kupumua ndio kipaumbele:WHO

Zaidi ya mahujaji milioni 2 wa Kiislam wanatarajiwa kushiriki katika shughuli za Hijja zinazooanza wiki ijayo kwenye mji mtakatifu wa Mecca Saudia.

Katika maandalizi wizara ya afya ya Saudia kwa msaada wa shirika la afya duniani WHO wameandaa hatua za kuzuia na kushughulikia haraka matatizo yoyote ya kiafya yatakayojitokeza wakati wa Hijja, ikiwa ni pamoja na virusi vya Corona na maradhi mengine ya kupumua.

WHO pia imechangia katika kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya 25 kutoka Jeddah, Mecca na Madinah ili kukabiliana haraka na dharura zozote zinakazoibuka za kiafya. Rana Sidani ni msemaji wa kanda ya Mashariki na Mediterranean wa WHO ambaye kwa sasa yuko , Mina Saudi Arabia.