Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Afrika ya Kati apongeza mbinu za kisheria Gabon

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Afrika ya Kati apongeza mbinu za kisheria Gabon

Mwakilishi maalum wa katibu mkuu Umoja wa Mataifa kwa Afrika ya kati Abdolaye Bathily amesema ameridhishwa na hatua iliyochuliwa na kiongozi wa upinzani nchini Gabon Jean Ping ya kukata  rufaa mahakama ya kikatiba kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi wa uraisi nchini humo. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

Bwana Bathily amepongeza mbinu za kisheria zilizotumika kutafuta muafaka huku akisisitiza kuwa mchakato huo unaonyesha ukomavu wa viongozi katika jitihada za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro uliozuka baada ya kutangazwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa uraisi mwezi uliopita ambapo Rais Ali Bongo Ondimba alitangazwa mshindi.

Kwa mujibu wa mamlaka yake, Mwakili huyu anasema ana amini  kuwa mahakama kuu ya Gabon itafanya uamuzi  kwa uaminifu na uwazi huku ikifuata misingi demokrasia  ya katiba ya Gabon.

Amepongeza jumuiya ya kiuchumi ya Afrika ya Kati na muungano wa Afrika na jamii ya kimataifa kwa kuendelea kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mchakato huo huko Gabon.