Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya Wanaigeria warejea nyumbani Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo:UNHCR

Mamia ya Wanaigeria warejea nyumbani Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo:UNHCR

Mamia ya wakimbizi wa ndani wanarejea katika vijiji vyao na miji iliyokombolewa hivi karinbuni na jeshi la Nigeria Kaskazini Mashariki mwa jimbo la Borno.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema linatarajia idadi yao kuongezeka katika wiki zijazo, lakini linasalia kuwa na hofu kuhusu mustakhbali bwao hasa maeneo yanayodhibitiwa na Boko Haram.

Msaada wa serikali na mashirika ya misaada umeimarishwa ili kusaidia wilaya 16 zinazofikika hivi sasa ambako watu Zaidi ya 800,000 wanahitaji msaada wa haraka. Leo Dobbs ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA DOBBS)

“Wengine wao wanaorejea makwao wanaokana ni wenye furaha  kwani wanasema walipokuwa hali ni mbaya zaidi, lakini bado tuna wasiwasi mkubwa  na ustawi wa watu hawa wanaorejea na tunawasiwasi na upataji wa habari kuhusu hali katika maeneo wanayorejea na huduma watakazopata”