Skip to main content

IAEA na jaribio la nyuklia huko DPRK

IAEA na jaribio la nyuklia huko DPRK

Jaribio la nyuklia lililoripotiwa kufanywa leo na Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK iwapo litathibitishwa, litakuwa ni la pili mwaka huu na la tano tangu mwaka 2006.

Ni kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA Dkt. Yukia Amano kufuatia ripoti hizo za jaribio akisema ni kinyume na maazimio kadhaa ya baraza la usalama ikiwemo lile namba 2270.

Huu ni ukiukwaji dhahiri wa maazimio kadhaa ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,  na ni upuuzaji wa wito wa mara kwa mara wa jamii ya kimataifa. Jambo hili linatia shida na ni la kusikitisha.”

Amesema IAEA inafuatilia kwa karibu suala la nyuklia la DPRK na iko tayari kusaka suluhu kwa kurejelea shughuli za ufuatiliaji wa mipango ya nyuklia pindi makubaliano ya nchi husika yatakapokamilika.