Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi zaidi wa Sudan Kusini waingia DRC- MONUSCO

Wakimbizi zaidi wa Sudan Kusini waingia DRC- MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO imearifu kuwepo kwa wakimbizi wa Sudan Kusini wapatao Elfu 20 kwenye eneo lililokuwa awali, jimbo la mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa MONUSCO Felix Prosper Basse amesema, yasemekana wakimbizi hao wamekimbia mapigano mapya nchini mwao.

Ghasia nchini Sudan K usini zimeanza mwezi Disemba mwaka 2013 na hadi sasa bado kuna mapigano na Umoja wa Mataifa umeridhia jeshi la kikanda la ulinzi ambalo tayari serikali imekubali.

Kikosi hicho kitakuwa na askari elfu nne kutoka nchi za ukanda huo wa Afrika.