Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutokua na uamuzi kumeturudisha nyuma-Mogens

Kutokua na uamuzi kumeturudisha nyuma-Mogens

Kile wanachokiona, kwa bahati mbaya ni kweli, hayo ni maneno ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mogens Lyketofft wakati wa mahojiano na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, wakati huu anapokaribia mwisho wa ng’we yake.

Kituo hicho cha habari kilitaka kufahamu kutoka kwa Mogens mtazamo wake juu ya hoja kuwa Umoja wa Mataifa, haufanyi kazi ya kutosha katika dunia hii iliyoghubikwa na vita na hali duni ya kibinadamu.

(Sauti ya Mogens)

"Bila shaka tunafanya mambo mengi mazuri katika oparesheni za kulinda amani duniani kote, lakini baadhi ya migogoro mikubwa zaidi kama ya Syria, Yemen, Sudan Kusini, hatuwajaweza, kwani hatuna  uamuzi- yaani nguvu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa,  katika kukabiliana nayo kwa mafanikio, na hilo limezidisha mno majanga ya kibinadamu na idadi ya kipekee ya wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao.