Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapiganaji wa SPLA-IO Sudan Kusini waingia DRC

Wapiganaji wa SPLA-IO Sudan Kusini waingia DRC

Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa baadhi ya wapiganaji wa kikundi cha Sudan People Liberation Army, cha upande wa upinzani huko Sudan Kusini, SPLA-IO wamevuka mpaka na kuingia Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC.

Msemaji wa umoja huo, Stéphane Dujarric amesema kuwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO umetumia misingi ya kibinadamu kuwaondoa baadhi ya wapiganaji majeruhiwa na kwamba..

(Sauti ya Dujarric)

“Tumewasiliana na mamlaka husika huko DRCongo na tunasisitiza tena kuwa wapiganaji hao wa SPLA upande wa upinzani wamepelekwa hospitali kwa misingi ya kibinadamu. Hali za wengi wao zilikuwa nni mbaya na ilikuwa ni suala la uhai au kifo na nafiriki ililazimika tuzingatie misingi ya kibinadamu, hatukuwa na njia nyingine.”

Wapiganaji hao wa kikundi cha SPLA upande wa upinzani wanamuunga mkono makamu wa kwanza wa zamani wa rais Sudan Kusini, Riek Machar ambapo Dujarric amesema kuwa wamepokonywa silaha zao lakini…

“Umuhimu wa mchakato wa kisiasa na amani nchini Sudan Kusini bado unasalia.  Hoja kuhusu dhima ya Riek Machar, au hali yake ya kiafya ni nini hiyo siwezi kujibu. Lakini kwa ukweli kabisa kama ni yeye binafsi au wawakilishi wake wa kisiasa kila mtu ana jukumu la kutekeleza ikiwemo serikali, ili kujaribu kurejesha pamoja Sudan Kusini.”