Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO na Google wasaidia watoto kujua kusoma Tanzania

UNESCO na Google wasaidia watoto kujua kusoma Tanzania

Nchini Tanzania kumefanyika maadhimisho ya siku ya kisomo ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limesema linatekeleza miradi ya kusaidia kuinua kiwango cha kusoma na kuandika miongoni mwa jamii kama vile wamasai. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Tumbuizo hilo la watoto wasioona kutoka shule ya msingi Uhuru mchanganyiko nchini Tanzania.. ni katika maadhisho ya siku ya kisomo jijini Dar es salaam.

Siku hii takwimu zimewekwa bayana kuwa kiwango cha kusoma hasa kwa watu wazima kiko chini na hivyo UNESCO ina miradi kadhaa ikiwemo kuwezesha jamii ya kimasai kujua kusoma na kuandika huko Ngorongoro, Olulosukwani.

Halikadhalika wamelenga watoto kupitia mradi wa EXPRISE ambapo watoto watajifunza bila mwalimu kupitia kifaa cha kisasa  au TABLET ambapo..

(Sauti ya Faith)