Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujua kusoma na kuandika ni msingi wa kufanikisha SDGs-Ban

Kujua kusoma na kuandika ni msingi wa kufanikisha SDGs-Ban

Miaka 50 tangu kuanza maadhimisho ya siku ya kujua kusoma na kuandika duniani, maendeleo mengi yamefikiwa lakini bado kuna changamoto kwa kila mtu kujua kusoma na kuandika.

Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kisomo duniani  hii leo, akisema kuwa hivi sasa zaidi ya watu milioni 750 duniani kote, ni wajinga wa kutokujua kusoma na kuandika, theluthi mbili ya hao ni wanawake, na vikwazo vikubwa vya maendeleo vinapatikana katika Afrika .Taarifa zaidi na Rosemary Musumba.

(Taarifa ya Rosemary)

Katibu Mkuu amesema kati yao hao milioni 115 ni vijana, na hivyo kuwa ni kikwazo katika kufanikisha ajenda 2030 ambayo kwayo kujua kusoma na kuandika ndio kitovu chake.

Kwa mantiki hiyo amesema vikwazo hivyo kwa maendeleo endelevu vinaweza kuondolewa kwa kutunga sera sahihi zinazopatiwa kichochea na rasilimali za kutosha.

Mathalani amesema ni lazima kuhakikisha watoto ambao hawako shuleni wanapata fursa ya kujifunza, sambamba na kuboresha elimu inayotolewa na kuendeleza elimu ya watu wazima.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi  na utamaduni, UNESCO Irina Bokova ameunga mkono kauli ya Katibu Mkuu Ban kuwa kisomo ndio msingi wa kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu