Skip to main content

Ban akutana na watumiaji madawa ya kulevya na familia zao Laos

Ban akutana na watumiaji madawa ya kulevya na familia zao Laos

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametembelea kituo cha matibabu dhidi ya madawa ya kulevya huko Ventiane, Laos, wakati wa ziara yake nchini humo alikohudhuria mkutano wa pamoja wa viongozi wa umoja wa mataifa na umoja wa nchi za kusini-mashariki mwa Asia, ASEAN.

Kituo hicho kilicho karibu na jamii kimeanzishwa kwa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Laos, na kinatibu waathirika wa dawa za kulevya.

Eneo la Vientiane ndilo lililoathirika zaidi kutokana na ongezeko la dawa ya kulevya aina ya Methamphetamine [METHA-M-PHETAMIN] au Meth, yenye bei nafuu zaidi.

Awali akishiriki mkutano wa ASEAN, Katibu Mkuu amegusia pia suala la haki za binadamu na uhusiano wake na ajenda 2030 na mkataba wa Paris..

(Sauti ya Ban)

Ningependa pia kuhamasisha viongozi kusaka usawa, ujumuishi na uwajibikaji katika serikali na jamii zenu. Ni lazima tuangalie njia za kujumuisha haki za binadamu katika maeneo yote ya udau wa ASEAN na Umoja wa Mataifa.”