Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na USAID zakubaliana kukuza kilimo

FAO na USAID zakubaliana kukuza kilimo

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO na lile la maendeleo ya kimataifa la Marekani, USAID wamesaidi makubaliano ya dola Milioni 15 yenye lengo la kukuza uwezo wa nchi zinazoendelea kufuatilia takwimu muhimu za  kilimo.

Takwimu hizo zitasaidia katika kutunga sera zinazowezesha kufanikisha lengo namba mbili la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ambalo ni kutokomeza njaa, kufanikisha upatikanaji wa chakula na kuendelea kilimo endelevu.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO Jose Graziano Da Silva amesema  katika miongo ijayo, kuna umuhimu wa kuzalisha chakula kwa uendelevu zaidi kwa  kwa kutumia rasilimali za asili kama vile maji na bayonuai kwa njia endelevu wakati huu wa mabadiliko ya tabianchi.