Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima tubadili mkakati wetu dhidi ya waasi DRC- MONUSCO

Lazima tubadili mkakati wetu dhidi ya waasi DRC- MONUSCO

Usiku wa tarehe 13 ya mwezi uliopita, wakazi wa kijiji cha Rwangoma, kwenye mji wa Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC walikumbwa na mashambulizi yaliyosababisha mauaji ya vifo vya watu zaidi ya 50 na majeruhi kadhaa. Umoja wa Mataifa ulilaani vikali shambulio hilo lililofanywa na waasi wa ADF. Naye mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis alilaani shambulio hilo ambapo hivi karibuni mwakilishi wake huko DRC, alitembelea akiambatana na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa. Je nini kilijiri? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.