Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa wahamiaji na wakimbizi kuibuka na azimio

Mkutano wa wahamiaji na wakimbizi kuibuka na azimio

Ukubwa wa tatizo la wakimbizi na wahamiaji barani Ulaya, umelazimu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kukutana jijini New York, Marekani  tarehe 19 mwezi huu ambapo wajumbe watapitisha azimio la New York. Azimio hilo linalenga kuongeza ulinzi kwa maelfu ya wahamiaji na wakimbizi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema kwa mara ya kwanza katika historia ya umoja huo, nchi wanachama 194 wanakutana kujadili na kuazimia jinsi ya kutatua tatizo hilo kubwa.

Melissa Flemming, msemaji wa UNHCR anasema mkutano huo na azimio hilo vina maana gani..

(Sauti ya Melissa)

“Mara baada ya kupitishwa, tunaamini kuwa itakuwa hatua muhimu sana, kwani mataifa 194 yatakayosaini azimio hili yatatangaza kwanza mshikamano wao mkubwa kwa watu wanaolazimika kukimbia makwao, pili, watathibitisha majukumu yao ya kuheshimu haki za wakimbizi na wahamiaji na mataifa kutoa ahadi ya msaada imara kwa nchi zilizoathirika zaidi na tatizo hili”

Naye msemaji wa shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM, Leornard Doyle amesema huu ni mkutano muafaka kwa IOM ambayo hatimaye inatambuliwa kama sehemu ya Umoja wa Mataifa na kwamba....

(Sauti ya Leornard)

“Hii ni muhimu sana kwani mambo yamebadilika sana, sasa kunatambulika kwamba kila nchi inahitaji kupambana na suala la wahamiaji kwa busara, kiutu uzima, na kwa njia inayotekelezeka.