Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Warsha yaangazia matumizi ya nyuklia kudhibiti mbu

Warsha yaangazia matumizi ya nyuklia kudhibiti mbu

Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA, linaendesha warsha huko, Kuala Lumpur, Malaysia kujadili njia mbadala za kutumia nishati ya nyuklia kukomesha mbu wanaoeneza virusi vya Zika, na vile vya magonjwa mengine kama dengue, chikungunya na homa ya manjano. Brian Lehander na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Brian)

Ikiwa imeandaliwa kwa ubia na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO, warsha hiyo ya wiki moja imewaleta pamoja wanasayansi na wataalam wa mambo ya afya kutoka nchi 40 za bara la Asia, Amerika na Afrika kwa lengo la kujifunza mbinu ya STI inayodhibiti mbu kuzaliana.

Mbinu hiyo ni safi kwa mazingira ambapo wataalamu wa IAEA wamesema utafiiti unaonyesha kuwa maambukizi kutoka kwa mbu yanasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani, hiyvo kuhatarisha maisha ya karibu watu bilioni moja  hasa bara la Asia na Afrika.

Wamesema ukosekanaji wa  chanjo, na kutopatikana kwa dawa kiurahisi, njia hiyo ya kudhibiti mbu kuzaliana ni muhimu zaidi wakati huu.